Nigeria imefanikiwa kukata tikiti ya kucheza katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil . Nigeria iliishinda Ethiopia kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa pili wa mtoano na kupata ushindi wa jumla ya mabao 4-1.Nigeria imechukua nafasi ya kwanza kati ya tano zilizotengwa kwa bara la Afrika katika kinyang'anyiro hicho mwakani, na kufuatiwa na Cote D'Ivoire ambayo ilifanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 na Senegal jana Jumamosi. Cote D'Ivoire imefanikiwa kukata tikiti hiyo kwenda Brazil kwa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya Senegal.Katika nafasi tatu zilizobaki kwa bara la Afrika , Cameroon na Tunisia na Burkina Faso na Algeria zinatarajiwa kupambana leo jioni.
Misri itaikaribisha Ghana katika mpambano utakaofanyika siku ya Jumanne, utakaokamilisha jumla ya timu tano kutoka bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment