Leo
November 16 2013 ni siku ya kuzaliwa ya Marehemu Albert Mangweha
(Ngwea) ambae May 28 2013 alifariki akiwa Afrika Kusini alikokwenda
kufanya showz kwenye miji mbalimbali ya nchi hiyo ikiwemo Johannesburg
na Capetown.
Usiku wa November 16 2013 umefanyika mkesha nyumbani kwao Morogoro na kufuatiwa na ibada Kanisani ya kumkumbuka Albert ambae alikua ni staa wa bongofleva mwenye rekodi ya kuwa na hits nyingi kuanzia anaanza muziki mwaka 1996.
Yafuatayo ni mambo matano yanayomuhusu Marehemu Albert ambae alizikwa kwao Morogoro.
1. Alianza kurap mwaka 1996 kwa kurudia nyimbo za mastaa kama B.I.G ambae ndio alikua msanii wa kwanza anaemkubali, mwaka huohuo ndio Ngwea alianza kuandika mashairi na hapa namkariri akisema ‘ndio zilezile kiburi jeuri tulia tuli msuli….. si unajua zile mradi umetoa vina lakini maana yenyewe teble!!! hahahahhahah, nomaa ‘
2. Ngwea ni Mngoni wa Songea lakini alizaliwa Mbeya November 16 1982 alafu mwaka 1987 wazazi wakahamia Morogoro baada ya hapo mwaka 1994 akahamia Dodoma kwenda kusoma.
3. Alipokua akisoma Mazengo ndipo alikutana na Dark Master, Mez B na Noorah na anasema Chemba ndio imezaliwa kule japo ilianzishwa na Tino Mkale, Mgulu George na wengine.
4. Kabla ya hapo kulikua na utofauti kwenye kundi lao la Chemba, walikua na kundi linaitwa CFG yani Chemba Fleva Guys lililoundwa na Ngwea mwenyewe, Mez B na Nzeku hivyo walivyomaliza shule ikabidi waondoe tofauti wakaamua kuiendeleza Chemba.
5. Ngwea kama Solo Artist alifanya bonge la party nyumbani Morogoro sehemu inaitwa Shimoni, Disco ambalo Ngwea alikiri ndio limemlea ambapo kwenye party alijumuika na kina O Ten, John Dilinga, Squizer, Dudubaya na wengine, namkariri akisema ‘enzi hizo kucheza lazima upige msamba lakini mpaka sasa hivi bado tunakimbiza farasi… 100′
Huyu ni Kaka wa Marehemu.
B12 @Bdozen wa XXL CloudsFM alikua miongoni mwa walikutana na kusafiri mpaka Morogoro nyumbani kwa kina Ngwea.
Young Dee ni miongoni mwa wasanii waliokuwepo kwenye mkesha, alisafiri pamoja na kina B12.

No comments:
Post a Comment