Hii ni kwa wateja wote wanaopata huduma ya umeme kupitia gridi ya taifa, imetangazwa kupata adha ya
mgao wa umeme kwa mwendo wa siku 11 kuanzia hivi leo kutokana na upungufu wa gesi itokayo katika kisiwa cha songosongo kilichopo wilayani kilwa mkoani Lindi.
Hali hiyo imesababishwa na kuwapo kwa matengenezo ya kiufundi katika visima vya gesi unaofanywa na kampuni ya PAT (Pan African Energy Tanzania Limited). Meneja mahusiano TANESCO Badra Masoud alisema hayo jana jijini Dar es salaam, amesema tatizo hili la umeme litakuwa katika kipindi cha Novemba 16 hadi Novemba 26 mwaka huu. itahusisha maeneo yote ya mikioa iliyo unganishwa na gridi ya taifa.
"tumepata barua kutoka kampuni ya Pan African inayotuuzia gesi, wakisema inafanya matengenezo hayo kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo. Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme" alisema
Pia aliitaja mikoa na maeneo yatakayo kumbwa na mgao wa umeme kama ifuatavyo;
Dar es salaam, Pwani, Tanga. Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida, Mwanza, Mara, Mbeya,
Iringa, Tabora, Shinyanga, Manyara na Zanzibar
No comments:
Post a Comment